ZANZIBAR INAHITAJI WATAALAMU MBALIMBALI KATIKA KUKUZA MAENDELEO YA SEKTA ZA KIUCHUMI NA KIJAMII.

Waziri wa  fedha na mipango dk halid  salum mohamed  amesema zanzibar  inahitaji wataalamu mbalimbali katika kukuza maendeleo ya sekta za kiuchumi na kijamii.

Amesema bila ya juhudi hizo taaluma walizozisomea zitakuwa hazina tija hasa kwa  wahitimu wa chuo cha utawala wa umma wanaotegemewa katika kusimamia mabadiliko  ya utawala   wa umma.

Akizungumza  katika  mahafali  ya tisa  ya  chuo hicho  amewasisitiza  wahitimu  hao  wa ngazi  ya  cheti na stashahada  kubuni  njia na  fursa  za  kujiajiri wenyewe na kuacha  dhana ya kutegemea ajira  serikalini pekee.

Katika  risala  ya wahitimu wa  chuo  hicho  iliyosomwa na   ndugu  abdul –karim   abubakar  ameeleza miongoni  mwa  changamoto  ambazo  zinawakabili  ikiwemo   ubovu  wa  barabara ya kufikia  chuoni  kwao.

Akifafanua  kozi  zinazosomeshwa  chuoni  hapo mkurugenzi  wa  chuo  hicho bi  harusi  masheko  amesema  chuo hicho  kinasomesha  kozi  mabalimbali  zinazowapa  fursa  wanafunzi hao  ya  kujishughulisha  na   vitu tofauti  katika  jamii.