ZANZIBAR KUDHIBITI UHARIBIFU WA MAZINGIRA

 

 

 

Zanzibar itaweza kudhibiti uharibifu wa mazingira iwapo wananchi watabadilika na kuachana na   matumizi ya mkaa na kuni na kutumia nishati   mbadala   ya gesi.

Kauli   hiyo   imetolewa  na baadhi  ya  wananchi  wa jimbo la  tunguu   baada   ya   kupokea   mitungi  ya   gesi,  majiko  sanifu  yanayotumia    gesi na  vifaa   vyengine  vya  matumizi  ya   nyumbani    vilivyotolewa   na    viongozi  wa    jimbo    hilo.

Wamesema  vifaa   hivyo  vikitumika  ipasavyo vitanusuru  msitu   kukatwa  kwa  ajili  ya   kuni  pamoja  na  kuepusha  nchi  kuwa  jangwa  pia  kupunguza  gharama   za   maisha  kwa  wananchi  wa   kipato   cha     chini .

Akizungumza baada  ya kushuhudia  makabidhiano    hayo    mwenyekiti   wa  ccm  wa  mkoa  wa   kusini   abadalla   ali   amesema  uhifadhi  wa    mazingira   ni  moja    ya  eneo   lililopewa  kipaumbele  katika   ilani   ya     chama   hicho    na  kuwasisitiza  wakaazi  wa   jimbo   hilo   kuunga   mkono   juhudi  za   viongozi    wao.

Mwakilishi   wa   jimbo la   tunguu   simai    mohammed    na   mbunge   khalifa    suleimani    wamesema   utoaji   wa    vifaa   hivyo    ni   mkakati   maalum     wa   kuwapunguzia  ukali  wa  maisha   wananchi   pia  unalenga    kuhakikisha  mazingira   yanabaki  salama   na   endelevu.