ZANZIBAR KUFIKIA KIWANGO KILICHOPEWA NA SAUDI ARABIA KUSAFIRISHA MAHUJAJI

 

Zanzibar imejipanga kufikia kiwango kilichopewa na saudi arabia cha kusafirisha mahujaji elfu mbili na mia tano wa tanzania kila mwaka kinyume na sasa ambapo sasa si zaidi ya mahujaji elfu mbili na mia tano wanaotekeleza ibada hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mashehe, wanazuoni na maulamaa mbalimbali wamesema kutofikiwa kwa kiwango hicho kunachangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo gharama kubwa za safari pamoja na kutohamasika kwa jamii kutekeleza ibada hiyo.

Wadau hao walikuwa wakizungumza katika kongamano la ufunguzi wa huduma ya hijja kupitia benki ya kiisalamu ya pbz ambapo wameziomba taasisi zinasofarisha majujaji kubuni mbinu mpya ambazo zitapunguza gharama na kuwawezesha wasilamu wengi kumudu kutekeleza ibada ya hija.

Meneja wa benki ya kiislamu pbz said mohames said amesema kwa kutambua umuhimu wa ibada ya hija benki hiyo imeanzisha huduma za kuwasafirisha mahujaji kupitia huduma ya akiba ambayo itamuwezesha mtu kuchangia kidogo kidogo hadi kukamilika fedha zinazohitajika pamoja na huduma nyengine ya kusafiriswha na kulipia baadae ambapo misingi ya kiislamu imezingatiwa.

Kongamano hilo limefunguliwa na mufti mkuu wa zanzibar sheikh saleh omar kabi ambapo ameshukuru wazo la benki hiyo kuanzisha huduma hiyo ambayo inalengo la kuongeza mwamko kwa waislamu kutekeleza ibada ya hija.