ZANZIBAR KUINUA VIPAJI MASKULINI

Baraza la michezo la taifa zanzibar,[btmz] wakishirikiana na idara ya michezo lnaendelea kutoa mafunzo kwa walimu skuli mbalimbali katika mchezo wa mpira wa miguu zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya mchezo huo.
Mafunzo hayo ya miaka 2 mfululizo yenye lengo ya kuisaidia zanzibar katika kuinua vipaji maskulini yaliotolewa tolewa na wakufunzi wa coach kross kontinet.
Kwa kuwafundisha waalimu wa skuli za unguja na pemba, jumla ya walimu 70 walio hudhuria mafunzo hayo kwa wilaya zote za unguja na baada ya wiki moja mafunzo hayo yanafanyika pemba kwa kushirikisha wilaya zote .
Mkurugenzi idara ya michezo hassan hairalwa amesema lengo limefanikiwa walimu waliopewa mafunzo ya kimaishan maisha uwezo wa kufundisha, pia kuwaomba kamati ya walimu wakuu wazazi na wadau kumuunga mkono rais wa zanzibar azima yake kuinua michezo nchin.
Mwenyekiti wa [btmz] amesema wao ni juukumu lao kama serekali kutoa mafunzo na kuweka miundombinu sawa ya viwanja anbayo rais wa zanzibar ameanza kutekeleza kwa kuanza kujenga kiwanja cha kitogani katika mkoa wa kusini unguja.
Nao washiriki walio pata mafunzo hayo wamesema bila ya mafunzo hawawezi kuibua vipaji na watakuwa makini juu ya elimu wanayo ipata .