ZANZIBAR KUONDOKANA NA MARADHI YA MIRIPUKO WAKATI WA MISIMU YA MVUA

 

Katika kuhakikisha zanzibar  inaondokana na maradhi ya miripuko wakati wa misimu ya  mvua  vijana wa taasisi ya hima hima wameandaa zoezi maalum wa ukusanyaji wa taka katika mji wa zanzibar.

Mwenyekiti wa taasisi hiyo ndugu othman kibwana na mjumbe nadra juma muhamed, wakishiriki zoezi la uzowaji taka ,wamesema hatua hiyo itasaidia kuondosha mlundikano wa taka katika  meneo mbali mbali .

Amesema  zoezi hilo  litakuwa endelevu kwenye  majimbo yote ya mkoa wa mjini magharibi .

Mwakilishi wa jimbo la pangawe mh. Khamis juma mwalimu amesema ni vyema kwa wakaazi wa jimbo hilo kubadilika ili kuhakikisha wanaweka mazingira safi  katika maeneo yao.

Wakizungumza  na zbc sheha wa shehia ya pangawe ali abdallah mtumweni na wakaazi wa shehia hiyo wameipongeza taasisi hiyo ya hima hima kwa uamuzi huo na kuitaka jamii kuacha tabia ya utuaji taka ovyo .

Shehia zilizofanyiwa zoezi hilo ni pangawe,kijitoupele, kinuni,mwembemajogoo na kijitupele ambapo liliwashirikisha madiwani,mabaraza ya vijana ya shehia.