ZANZIBAR KUSHIRIKIANA KIBIASHARA NA NCHI TOFAUTI

Zanzibar   hivi sasa  inaendelea   katika  masuala  ya kiuchumi   hivyo  ipo  haja  ya   kushirikiana kibiashara  na  Nchi  tofauti  ikiwa  pamoja na  uimarishaji wa  miundombinu ya  kibiashara ili  kuweza  kufikia adhma  hiyo .

Akizungumza katika  uzinduzi  wa maonesho ya  baadhi  ya bidhaa  za  india ikiwa  ni  miongoni  mwa  kukuza  uhusiano  wa  kibiashara  naibu  Waziri  wa biashara  na  viwanda  Mh  Hassan  Hafidh  amesema hali  hiyo  itasaidia  kurudisha  hadhi  ya  kibiashara  iliopo  awali   na  kuweza  kujiimarisha  zaidi  katika  uchumi  wa  viwanda ili  kufikia  uchumi  wa  kati.

Balozi  wa  india  Nchini  Tanzania bwana  Sandeep Arya amesema    Nchi  yake  imeamua  kutoa  upendeleo  maalu m  wa  ushuru   kwa  bidhaa   kwa  baadhi  ya  Nchi  ikiwemo  tanzania  pamoja  na  kufuta  gharama  za  viza  za  biashara kwa  wafanyabiashara wa  tanzania.

Nao  wafanyabiashara  waliohudhuriwa  uzinduzi  huo wamesema   wameomba   kufanyika  kwa  ziara  za  kupata  utaalamu  ikiwa  pamoja  na  wafanyabiashara  wa  nchini  india  kuja  Zanzibar  kwa  ajili  ya  kupeana  mbinu na uzoefu  wa kibiashara.

Mapema  Mh  Hassan alikagua  maonesho  ya  baadhi  ya  biashara  zinazoingia  hapa  nchini  kutoka  nchi  india ili  kuwa  ni fursa  moja  wapo  ya  kushirikiana  kibiashara  ili  nao   waweze  kupeleka  Nchini   India.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App