ZANZIBAR KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU YA UTI WA MGONGO

 

 

Zanzibar imefanikiwa katika kutoa huduma za matibabu ya uti wa mgongo, vichwa maji, na mishipa ya fahamu katika kipindi kifupi tokea kuanzishwa huduma hizo.

Mratibu wa mkutano wa wataalamu wa kutibu maradhi hayo kwa nchi za afrika ya mashariki dr. Mahamoud qureshi amesema zanzibar kupitia hospitali ya hospitali ya mnazimmoja ndio pekee inatoa matibabu katika jengo linalojitegemea kwa watu bila kujali uwezo wa kifedha.

Mkurugenzi  mkuu wa wizara ya afya dkt. Jamala adam amesema mkutano huo utasaidia kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa watendaji katika kukiimarisha kitengo kinachoshughulika na maradhi hayo.

Ameongeza kuwa kituo hicho si tu kinawanufaisha wananchi wa zanzibar bali hata nchi jirani hufuata huduma hiyo.

mkutano huo unamwenda sambamba na utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa kwa kutumia wataalamu wazalendo