ZANZIBAR KUZIENDELEZA TIMU ZAO ZILIZOKWENDA KWENYE MASHINDANO YA UMISSETA

 

Idara ya michezo na utamaduni wizara ya elimu na mafunzo ya amaali zanzibar imeanzisha mpango maalum wa kuziendeleza timu zao mbali mbali zilizokwenda kwenye mashindano ya umisseta mkoani mwanza mwezi june mwaka huu.

Mkurugenzi idara ya michezo na utamaduni kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali hassan khairalla tawakal amesema timu zote zilifokwenda kushiriki mashindano ya umisseta wataziendeleza hasa zile zilizofanya vizuri ikiwemo ya mpira wa meza iliyotwaa ubingwa na ya mpira wa mikono iliyoshika nafasi ya pili.

Amesema lengo la serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni kurejesha vugu vugu la michezo kama anavyotaka rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohammed shein.