ZANZIBAR KUZIFANYIA UTAFITI TAASISI BINAFSI ZILIZOKUWA HAZIJATIMIZA AGIZO LA SERIKALI LA KUONGEZA MISHAHARA

Katibu mkuu wa  shirikisho   la  vyama  huru  vya   wafanyakazi  Zanzibar   Zatuc  Khamis   Mwinyi  Mohamed  ameitaka   kamisheni ya  kazi  Zanzibar  kuzifanyia utafiti  taasisi binafsi kuzigundua  zilizokuwa hazijatimiza agizo la serikali la kuongeza  mishahara  kwa wafanyakazi wake.

Akizungumza na vyombo  vya  habari  nd  khamisi  amesema  kuna baadhi ya taasisi  zinadai kuwa kiwango  cha mishahara   kilichotajwa na serikali bado hakijawa  rasmin  hivyo wasubiri mazungumzo yanayoendelea baina yao na  serikali.

Aidha   Ndugu  Khamisi   ametoa shukrani kwa uongozi  wa Dr. Ali Mohammed Shein kwa hatua yake ya  kutangaza nyongeza ya mishahara   na  pencheni  kwa  watumishi wa umma.