ZATU KUFANYA TATHMINI KATIKA UONGEZWAJI WA MISHAHARA MIPYA KWA WAALIMU

chama cha waalimu zanzibar kimefanya tathmini katika uongezwaji wa mishahara mipya kwa waalimu na kugunduagua matatizo mengi ikiwa ni pamoja na kupunguzwa kwa posho ya ualimu.
akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa zatu mussa omar tafurwa amesema kwa kushirikiana na chama cha wafanyakazi na taasisi nyengine zinazohusika wanaendelea kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili walimu waweze kupata stahiki zao.
ameeleza kuwa mbali na tatizo hilo suala la kushushwa ngazi ambalo limewagusa wafanyakazi mbalimbali wa serikali linahitaji kupatiwa ufumbuzi kwani inachukua muda muajiriwa kupandishwa daraja.
katika hatua nyengine chama hicho kinatarajia kufanya uchaguzi kwa awamu ya tatu kuanzia mwezi ujao na kufikia kilele chake mwezi februar mwakani kwa kuanzia ngazi ya skuli, kanda hadi taifa.