(ZBC) KUWEKA MIKAKATI IMARA YA KUSOGEZA MAENDELEO YA VYOMBO

 

Kampuni ya azam media croup imesema ushirikiano wake na shirika la utangazaji zanzibar  (zbc)  utasaidia kuweka mikakati  imara ya kusogeza mbele maendeleo  ya vyombo hivyo.

Imesema chini ya ushirikiano huo azam media na zbc wanajipanga kuwaridhisha watazamaji wa vyombo hivyo sambamba na kujenga ushindani wa kihabari na vyombo vingine.

Mkurugenzi wa azam media group bwana tido muhando ameeleza malengo hayo katika kikao cha kuimarisha ushirikiano  wa kupeana uzoefu  katika  utendaji kati ya chombo hicho na  shirika la utangazaji  zanzibar  zbc .

Waziri wa habari  utalii na mambo ya kale mh, mahmoud thabit kombo amesema  ushrikiano huo utasaidia kuboresha utayarishaji wa vipindi vitakavyo  kubalika na jamii.

Naibu  katibu wizara ya habari utalii na mambo ya kale ndugu saleh mnemo amesema   ushirikiano wa pande mbili hizo utawezesha     wafanyakazi kufanyakazi vizuri.