ZBC LIMEAMUA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WAKE

 

Shirika la  utangazaji  zanzibar  katika  kuleta   mabadiliko ndani ya shirika hilo  zbc limeamua kuwajengea uwezo wafanyakazi wake ili kukabiliana  na changamoto  za kiutendaji.

Mkurugenzi  wa  shirika   nd.  Imane   duwe  akizungumza katika mafunzo kwa watendaji wa shirika hilo amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kwa muda  mrefu sasa wafanyakazi  hawajapatiwa   mafunzo  hali inayosababisha kufanya  kazi  kwa  mazowea.

Amesema mafunzo hayo yatawezesha  kwenda sambamba  na mabadiliko  ya  taasisi   katika  hatua  za  kufikia  watazamaji  na  wasikilizaji   kwa  karibu  zaidi .

Mtaalamu   mwelekezi   kutoka  sweden  mis   segebo  amesema  ipo  haja  ya  kutumika  mbinu   zitazoweza kukubaliana  kuzitumia kwa  lengo  la  kuleta  mabadiliko  ya  kiutendaji  kwa  mfumo  wa  shirika   huku  likizalisha zaidi.

Washiriki  wa  mafunzo  hayo  wamesema  licha  ya  kujengewa  uwezo   bado  wanahitaji  kuongezewa  vifaa   ili kukabiliana  na  mabadiliko .