ZBC RADIO RAHALEO KUFANYIWA MAREKEBISHO.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein ameagiza kufanyiwa tathmini ya matengendezo ya jengo la kurushia matangazo ya zbc radio rahaleo ili lifanyiwe matengenezo.

Akizungumza  katika ziara yua kulitembelea jengo hilo dr, shein amesema baadhi ya sehemu za jengo hilo ziko katika hali mbaya kutokana na kushambuliwa na mchwa na si vyema tatizxo hilo kuachwa hivyo  hivyo.

Amesema majengo ya vyombo vya habari yanahitaji kuwa na hadhi kutokana na umuhimu wake na serikali itaendelea kujitajitahidi kuyaboresha ili yalingane na vyombo vingine vya habari duniani.

Mkurugenzi mkuu wa zbc ndugu iman duwe  amesema pamoja na mafanikio yaliyokwisha  patikana na katika shirika lake lakini bado zipo baadhi ya changamoto ikiwemoya usafiri wa kutumia watendaji wake.

Mhariri mkuu wa zbc bi lulu mzee kari pamoja na mambo mengine  amempongeza dr, shein na serikali kwa jumla kwa juhudi zake za kuviendeleza vyombo vya habari vya serikali .