ZECO LIMEANZA KUFUNGA MITA ZA UMEME ZA KULIPIA ZA TUKUZA VIJIJINI

Shirika la umeme zanzibar zeco limeanza kufunga mita za umeme za kulipia za tukuza katika vijiji vitano vya mkoa wa kusini
Mpango huo umelenga kufikia vijiji vyote vya mkoa huo na kuanzia katika kijiji cha kizimkazi ambao zaidi ya nyumba mia tisa zitafungwa mita hizo
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha kizimkazi wameshukuru kwa kupatiwa mita hizo kwa kuwa na zitawaondolea hofu ya malipo pamoja na usumbufu waliokuwa wakiupata kwenda kulipa umeme mbali na kijiji chao.
Afisa uhusiano wa zecco salum abdalla hassan amesema ufungaji wa mita hizo ni muendelezo wa mpango wao wa kufikisha mita za tukuza kwa watumiaji wote wa umeme zanzibar ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa afisa huyo
Mara baada ya kumaliza kijiji cha kizimkazi mkunguni wataendele kizimkazi dimbani charawe ,muyuni ,muungoni na pete, zaidi ya mita mia tisa zinategemewa kufungwa katika vijiji hivyo