ZFA IMEFANYA KIKAO TOKA KUPITISHWA KUWA WANACHAMA 55 WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU

 

 

 

 

Leo hii kamati tendaji ya zfa taifa imefanya kikao chake cha mwanzo toka kupitishwa kuwa wanachama 55 wa  shirikisho la mpira wa miguu afrika.

Kamati hiyo kwa nguvu moja imempitisha rasmi  kocha Abdulghany Msoma kuwa mkurugenzi wa ufundi katika kikao ambacho kimefanyika leo hii majira ya saa 2:30 asubuhi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vyombo vya habari afisa habari wa zfa ALLY BAKARI [CHEUPE] taarifa juu ya malalamiko ya wachezaji ambao wanachezea bara juu ya kuichezea timu ya Zanzibar heros

Msoma baada ya kupatiwa nafasi hiyo amefurahishwa sana lakini amehimiza ushirikiano kati ya ZFA na wadau mbali mbali  ili kuinua mpira wa Zanzibar

Amesema ZFA bado hawajaweka sera rasmi, wajibu wangu mimi kuishauri ZFA katika swala hili sera rasmi kwa mpira jee Zanzibar tutaruhusu mambo haya na vipi tutashirikiana nayo.

Kwa mujibu wa makamu wa rais wa ZFA  Pemba ALI Mohammed akielezea baada ya kupatiwa uwanachama wa kudumu kutoka shirikisho la mpira barani afrika

 Wametakiwa kupunguza timu na kubakia na timu 12 kwa msimu ujao