ZFA IMEFUNGUWA RASMI KOZI YA UKOCHA NGAZI YA PRIMINARI

 

Makamu  wa  rais  zfa  kanda  ya  unguja  mzee  zam  ally leo  hii  amefunguwa  rasmi  kozi  ya  ukocha  ngazi  ya  priminari  katika  ofisi  za  zfa  wilaya  ya  magharibi ‘b’

Amewataka  makocha  hao  wachukuwe  bidii  katika  mafunzo  hayo  kwa  kutambuwa  kwamba  mpira  ni  ajira  hasa  kwa  kipindi  hiki  tulichokuwa  nacho Amewataka  makocha  kujiendekeza  kitaaluma  na kutoizembea  fursa  hiyo  ya kujiendeleza  katika  ellimu  na  fani  hiyo  ambayo  soko  lake  linashika  kasi  kila  siku duniani .

Mkufunzi  wa  shirikisho  la  mpira  wa  miguu   barani  afrika  caf    Nassra  Juma  ambae   ndie  mkufunzi  wa  kozi  hiyo  ya  priminari , amesema  mabadiliko  yatapatika  katika  mpira  wa  Zanzibar  iwapo  makocha  watakuwa  tayari  kujiunga  na  kozi  mbali  mbali  za  kimasomo  ya  mchezo  huo  zinazotolewa  na  chama  vya  mpira  wa  miguu .

Amesema  atatumia  ujuzi  wake  kuhakikisha makocha  hao  wanabadilika  na  kuleta  faida  ya  mchezo  huo  hapa  nchini.

PauseKozi  hiyo  imeandaliwa  na  zfa  wilaya  ya  magharibi  ‘b’  ambayo  inawashirikisha  makocha  thalathini  na  moja  kutoka  katika  wilaya  zote  za  Zanzibar.