ZFA IMESOGEZA MBELE ZOEZI LA KUTOA RASIMU YA KANUNI ZA MASHINDANO YA MSIMU MPYA WA MWAKA

Kamati teule ya chama cha soka visiwani zanzibar (zfa) imesogeza mbele zoezi la kutoa mapendekezo ya rasimu ya kanuni za mashindano ya msimu mpya wa mwaka 2018-2019 ambayo imehusisha mashindano kwa madaraja ya vijana hadi ligi kuu.

jumanne ndio ilikuwa siku ya mwisho kutoa mapendekezo ya rasimu hiyo lakini kutokana na wadau mbali mbali kuomba kuongezwa siku zoezi hilo, kamati imekubali ombi lao na kuongeza siku tatu hadi ijumaa ya agost 31, 2018 majira ya saa 6:00 za mchana.

Katibu wa kamati hiyo khamis abdallah said ame`wapongeza wadau wote walitoa mapendekezo yao kwa maandishi wakiwemo pia waandishi wa habari za michezo na vilabu ambao nao wamechangia kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.