ZIMAMOTO WALIENDELEA KUWASHA MOTO KWA KUCHEZA KABUMBU SAFI

 

 

Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na washabiki wa soka zanzibar wa klabu bingwa barani afrika ilipigwa   leo  katika  kiwanja  cha  amani  ambapo timu ya   zimamoto  ya  zanzibar  iliyovalia jezi rangi nyekundu walionesha umahiri wao katikia kulisakata kabumbu kwa kuwatungua timu ya  ferroviario  ya  msumbiji mabao 2-1 waqkati wa  saa  10 za jioni.

Mabingwa hao wa zanzibar zimamoto walitanguliwa kufungwa goli katika dakika ya kwanza tu ya mchezo wakati mchezaji manuel coreira alipopokea mpira wa haraka na kuujaza wavuni.

Zimamoto waliendelea kuwasha moto kwa kucheza kabumbu safi na mnamo dakika ya 33 ya mchezo khatib said aliisawazishia timu yake baada ya kupigwa mpira wa adabu uliomtoka mlinda mlango wa ferroviaro de beira na kuujaza wavuni kwa kichwa na kuzifikisha timu hizo mapumziko zikiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili tim u ya zima moto waliendelea kuliandama lango la wapinzani wao na ilipotimia dakika ya 65 mchezaji hakim khamis aliwanyanyua wapenzi wa soka waliohudhuria pambano hilo kwa kufunga bao la pili na la ushindi.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana baada ya wiki mbili huko nchini msumbiji.

Makocha wa timu hizo pamoja na washabiki walikuwa na machache ya kuongea kutokana na tathmini ya mchezo huo na matumaini katika mchezo wa marudiano.