ZIMBABWE ITAENDELEA KUIENZI TANZANIA KAMA NI MKOMBOZI WA NCHI HIYO

 

Rais wa jamhuri ya zimbabwe emmerson mnangwagwa amesema zimbabwe itaendelea kuienzi tanzania kama ni mkombozi wa nchi hiyo.Rais mnangwaga ambaye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi amefanya mazungumzo na mwenyeji wake rais john pombe magufuli ikili jijini dar-es-salaam na kumuhakikishia rais magufuli kuwa zimbabwe itaendeza mashirikiano yake na tanzania kama yalivyoasisiwa na hayati baba wa taifa mwalimu julius nyerere na rais wa kwanza wa zimbabwe robat mugabe.Amesema zimbabwe kama ilivyo nchi nyinginezo za kusini mwa  afrika itaendelea kuienzi tanzania kama mkombozi wa nchi hizo na kuhimiza viongozi na jamii za watu kukielezea kizazi cha sasa mchango huo  wa tanzania.

Naye rais magufuli amesema katika mazungumzo yao wamekubaliana kuzitumia fursa zilizopo katika nchi za sadec kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo, mifugo na uchakataji wa madini.Aidha rais magufuli akampongeza rais mnangwaga kwa kuonyesha ukomavu katika demokrasia na kumtaka kumuenzi rais mstaafu robati mugabe kama baba wa taifa la zimbabwe kutokana na mchango wake alioutoa katika kupigania uhuru wa nchi hiyo.Viongozi hao pia wamekubaliana kuvitangaza kwa pamoja vivutio vya utalii vilivyopo zimbabwe na tanzania badala ya kushindana ili kuwafanya wataalii wanatembelea  zimbabwe wafike pia tanzania na kuhitimisha ziara yao kwa kutembelea fukwe za zanzibar.

Mapema baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu julius nyerere rais mnangagwa alilakiwa na mwenyeji wake rais magufuli na kupokea salamu ya heshima kutoka kwa gadi ya jeshi la ulinzi la wananchi wa tanzania jwtz sambamba na kupigiwa mizinga 21.Kesho rais mnangagwa atatembelea  kijiji cha kaole wilayani bagamoyo mahali alipowahi kuishi wakati akiwa katika kambi ya wapigania uhuru ya frelimo mwaka 1963 na 64.