ZINEDINE ZIDANE AMESEMA ANAACHIA NGAZI REAL MADRID SIKU TANO

 

 

Zinedine zidane amesema anaachia ngazi real madrid siku tano baada ya kuwaongoza kushinda ligi ya mabingwa ulaya.zidane amezungumza na vyombo vya habari juu ya uamuzi wake huo.Anaondoka baada ya kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji matatu ya klabu bingwa na taji moja la ligi ya la liga tangu achukue hatamu mnamo mwezi januari 2016.Zidane, mwenye umri wa miaka 45, alichukua uongozi wa klabu hiyo baada ya rafael benitez kufutwa kazi na alisimamia mechi 149.Aliisaidia real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa. siku chache tu baada ya real kuishinda liverpool 3-1 katika fainali ya kombe la vilabu bingwa ulaya.