ZMA INATARAJIA KUTOA MUONGOZO WA USALAMA KWA VYOMBO VINAVYOFANYA SHUGHULI ZA UTALII

Mamlaka ya usafiri wa baharini zanzibar zma inatarajia kutoa muongozo wa usalama kwa vyombo vidogo vidogo vinavyofanya shughuli za utalii na uvuvi ili kuimarisha usimamizi wa baharini zanzibar.
Mkurugenzi wa huduma za bandari na meli z.m.a salma suleiman omar amesema muongozo huo utasaidia kuimarisha usalama wa vyombo vidogo vitakapokuwa baharini na kuepusha ajali
Muongozo huo utavihusu vyombo vinavyopakia abiria wasiopungua 20 na vinasafiri umbali isiozidi meli tano mapendekezo yake yamewasilishwa kwa wadau wa usafirishaji watalii, wavuvi na viongozi wa halmashauri.
Amefahamisha kuwa chombo chochote lazima kisajiliwe na zma wafanyakazi wake wawe na kibali maalumu, iwe na vifaa vya usalama na kiwe na alama maalumu kwa kazi inayofanya
Washiriki wa mkutano huo wameshauri kuwekwa kituo kimoja cha usajili wa vyombo vido vya baharini na kuwepo ushirikiano wa taasisi katika kusimamia taratibu ili kuhakikisha mapato yanayopatikana yanawasaidia wananchi.
Mkurugenzi kitengo cha usajili wa meli zma bi sheha ahmed mohammed akifungua mkutano huo amesema usajili wa vyombo vidogo unahitaji kutiliwa mkazo zaidi katika kuweka utaratibu wa kuwasaidia wamiliki wake ili kupata fidia wanapopata maafa baharini
Kwa mujibu wa mamlaka ya zma muongozo huo unatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni baada ya kukamilika taratibu za kisheria.