ZOEZI LA KUHESABU KURA LINAENDELEA LIBERIA

 

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyocheleweshwa nchini liberia, kumpata mrithi wa rais anayeondoka madarakani, mshindi wa tuzo ya amani ya nobel ellen johnson sirleaf.

Makamu wa rais joseph boakai anapambana na mchezaji wa zamani wa kandanda wa kimataifa george weah kuwania kiti hicho cha rais.

Wagombea wote wameapa kupambana na umasikini uliokithiri pamoja na rushwa nchini humo ambapo raia wengi hawana umeme wa kutosha pamoja na maji safi ya kunywa.

Uchaguzi huo wa duru ya pili, ambao unafuatia duru ya kwanza ya mwezi oktoba ulipangwa kufanyika novemba 7, lakini ulicheleweshwa kutokana na malalamiko ya udanganyifu wa uchaguzi yaliyochunguzwa na kutufutwa     na mahakama kuu.