ZOEZI LA ULAZAJI WA MABOMBA BAHARINI WILAYA YA WETE KUTOKAMILIKA KWA WAKATI

 

Wakaazi wa kisiwa cha kokota wilaya ya wete , wamesema mradi wa kupeleka maji unaweza  usikamilike kwa wakati kutokana na baadhi watu katika kisiwa hicho kutoshiriki zoezi la ulazaji wa mabomba  baharini.

Wakizungumza  na zbc , wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba  ya kukagua maendeleo ya mradi huo, baadhi ya wakaazi wa kisiwa hicho , akiwemo Suleiman Juma na Adam Said, wameitaka serikali kuwachukulia hatua wananchi wanaokaidi kushiriki zoezi hilo.

Aidha naye Juma Haji Juma ameishauri serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mradi huo, kabla ya kuchukua hatua za kisheria.

Katika  nasaha zake , mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba , mhe omar khamis othman amewataka wakazi wa kisiwa hicho, kuuthamini mradi huo ambao kukamilika kwake utawasaidia kuondosha usumbufu wanaoupata .

Mradi wa maji safi na salama katika kisiwa hicho unasimamiwa na shirika la milele foundation .