ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA HOSPITALI YA KIVUNGE

 

wanawake wanaokwenda hospitali ya kivunge kwa ajili ya kukaa na wagonjwa wao sehemu ya kujifungua kudumisha usafi katika maeneo hayo ili kujiepusha na maradhi.Ameyasema hayo baada ya kumalizika zoezi la usafi wa mazingira katika hospitali hiyo na kukabidhi zawadi kwa wanawake waliojifungua ikiwa ni shamrashamra ya kusherehekea siku ya wanawake.Amefahamisha kuwa hospitali ni sehemu kubwa ya mkusanyiko wa watu hivyo si busara kuwa katika hali ya uchafu hivyo amewashauri wanawake kudumisha usafi ili kuondosha mazalia ya mbu na wadudu watakaoweza kusambaza maradhi kutoka sehemu moja kwenda nyengine.Nae daktari dhamana wa hospitali hiyo bw: maulid abdallah khamis amewashukuru viongozi wa umoja wa wanawake kwa kuona umuhimu wa kufanya usafi katika hospitali hiyo.

Kwa upande wao viongozi wa umoja wa wanawake mkoa huo wamesema lengo la kufanya usafi katika kituo hicho ni kudumisha usafi katika kipindi hichio cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha ili kuendelea kupata huduma bora.