ZRB IMEFANYA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA KODI

 

Bodi ya mapato  zanzibar  zrb imefanya marekebisho ya sheria za kodi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ili kuleta ufanisi katika usimamizi wa kodi na kuhakikisha sheria zilizopo zinarahisisha utendaji wa kazi.

Akizungumza katika mkutano wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusiana na mabadiliko ya sheria ya ukusanyaji wa kodi kwa kutumia vifaa vya eletroniki  katika ukumbi wa zrb mazizini  mkuu wa kitengo cha mahusiano kwa umma bi safia ishaka mzee amesema  sheria zilizopo kabla zimeonekana  kupitwa na wakati na hazina  tija katika masuala ya kodi.

Amesema kutoakana  na mabadilko ya kiteknelojia na mifumo wa ukusanyaji kodi zrb  itaendelea kutoa taaluma juu ya mabadiliko hayo na kukuza utoaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa.

Akizitaja baadhi ya sheria zilizofanyiwa marekebisho bi safia amesema ni sheria mpya ya stempu ya mwaka 1996, sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka   2009,  na kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 1998.

Naye mkuu wa kitengo cha walipa kodi bw shaabani yahya ramadhani amesema mfumo wa  mashine za kieletroniki zitaiyongezea  serikali mapato katika ulipaji wa kodi