ZRB IMESEMA MABADILIKO YA SHERIA YA MAPATO IMESAIDIA KWA KULIPA KODI KWA WAKATI

 

Bodi ya mapato zanzibar zrb imesema hatua ya kuwashirikisha wadau katika mabadiliko ya sheria ya mapato kumesaidia kwa wafanya biashara kulipa kodi kwa wakati.

Akizungumza katika mafunzo ya sheria ya mapato mkuu wa kitengo cha sheria cha zrb khamis jaffar  amesema ulipaji kodi ni jambo la kisheria na ni kosa la jinai kwa atakayekwepa hivyo amewataka wananchi kulipa kodi bila kushurutishwa.

Meneja wa kodi zantel ndugu francis temba amesema kushirikishwa wadau katika sheria hiyo imetowa fursa ya uelewa  na kuonyesha  kuwajali wafanyabiashara .

Afisa uhusiano wa zrb ndugu makame amesema mabadiliko ya sheria hiyo mpya, yaliyofanyika yamekusudia kupunguza usumbufu kwa walipa kodi na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji.