ZRB IMEWATAKA WAANDISHI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA MABADILIKO YA SHERIA YA ULIPAJI KODI .

Bodi ya mapato zanzibar zrb imewataka waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi juu ya mabadiliko ya sheria ya ulipaji kodi nchini .
Akizungumza na waandishi wa habari wa katika ukumbi wa maktaba kuu b chake chake pemba meneja sera mipango na utafiti ahmed saadat amesema maeneo mengi ya marekebisho katika sheria ya usimamizi wa kodi ya namba 7 mwaka 2009 yamelenga kufanya mabadiliko ya vifungu vya sheria ili kuweza kukidhi haja ya uazishwaji wa utaratibu wa utoaji wa risiti.
Kwa upande wake nd shaaban yahya ramadhan amesema kufutwa kwa sheria ya stemp namba 6 mwaka 1996 na kuanzishwa sheria mpya ya ushuru wa stemp imelenga kuboresha usimamizi na kuondoa changamoto na kuboresha utoaji wa huduma
Akizungumza katika mafunzo hayo kaimu mkuu wa idara ya habari maelezo pemba kauthar ishak amewasisitiza waandishi hao kuitumia vyema elimu waliopewa kwa wananchi ili kufikia malengo yalio kusudiwa
Miongoni mwa sheria zilizofanyiwa marekebisho ni pamoja na sheria ya usimamizi wa kodi namba 7 ya mwaka 2009 sheria kodi ya ongezeko la thamani namba 4 ya mwaka 1998 pamoja na sheria ya mafuta namba 7 ya mwaka 2001