ZRB ITAENDELEA KUTHAMINI MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WASTAAFU WANAOMALIZA

 

 

Kamishna wa bodi ya mapato zanzibar zrb nd.amour hamil bakar, amesema zrb itaendelea kuthamini michango iliyotolewa na wastaafu wanaomaliza muda wao wa utumishi.Akizungumza katika hafla ya  kuwaaga wastaafu  waliomaliza muda wao  ndugu amour amesema kila penye mafanikio ya zrb wastaafu hao wameshiriki kikamilifu.

Amewataka wafanyakazi kuiga mifano mema ya utendaji wa kazi  walioyoiacha ili kuendelea kufanya kazi kwa bidii na  kuongeza ufanisi wa utendaji.Wakitoa shukurani wastaafu hao kwa  niaba ya wenzao  wamewashauri wafanyakazi waliopo kufanya kazi kuwa waadilifu ili kufikia hatua nzuri na kuweza kustaafu bila kuonekana na kasoro za kiutendaji.  Katika hafla  hiyo kamishna huyo amewakabidhi  wastaafu hao  zawadi za friji, jiko, vyarahani pamoja fedha taslim