ZRB KUKAMATA BIDHAA ZA SUKARI NA MAFUTA KWA NJIA MAGENDO

 

Bodi ya mapato zanzibar zrb imefanikiwa kukamata bidhaa za sukari na mafuta ya kupikia zilizokuwa zikitaka kusafirishwa kwa njia magendo katika bandari ya kisakasaka na kisiwa cha uzi.

Bidhaa hizo zikiwa ni polo zaidi ya mia tatu za sukari za ujazo wa kilo 50 na 25 na madumu ya mafuta 220 ya lita 20 yamekamatwa kwa ushirikiano wa zrb, jeshi la polisi na kikosi cha kuzia magendo kmkm zikitaka kuvushwa kwenda nje ya zanzibar.

Akielezea tukio hilo afisa dhamana kitengo cha uhusiano zrb bi safia is-haq mzee amesema bidhaa hizo zinazuiliwa hadi pale wahusika watakapokamilisha taratibu za kisheria ikiwemo kulipa gharama za kodi inayostahili pamoja na faini.

Amesema katika kukabiliana na magendo ya biashara ambayo yanalengo la ukwepaji wa kodi afisa huyo amesema wanaendlea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kutumia njia na bandari rasmi kusafirisha bidhaa badala ya kufanya udanganyifu.

Bidhaa zilizokamatwa zina thamani ya kiasi ya shilingi milioni 32.