ZSSF UMEFANYA UKAGUZI WA HATUA ZA UJENZI WA KATIKA JUMBA LA TRENI

 

Uongozi wa zssf umefanya ukaguzi wa hatua za ujenzi wa mradi wa nyumba ya biashara katika  jumba la treni darajani na kusema ujenzi huo utamalizika kwa wakati uliopangwa

Akiongoza msafara wa viongozi wa bodi ya zssf katika ukaguzi wa ujenzi huo mkurugenzi mwendeshaji wa zssf bw abdulwakil haji hafidh amesema hatua za mwanzo za  matayarisho kwa hatua za ujenzi huo zinaendelea vizuri ila kwa sasa wanachosubiri ni kibali cha ujenzi wa jengo lote kutoka  unesco

Nae mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya zssf bw suleiman rashid  amesema kwa upande wao kama bodi wamerishishwa na hatua zinazoendelea katika kulifanyia marekebisho makubwa na ya kisasa jengo hilo kongwe kuwa na umadhubuti.

Matengenezo ya mradi huo wa jengo hilo unatarajiwa kuchukua miezi  18 na kugharimu kiasi ya shilingi bilioni 8 hadi kukamilika kwake