ZSSF UMESEMA PAMOJA NA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIUTENDAJI,

 

Mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF umesema pamoja na kutekeleza majukumu yake ya kiutendaji,  itaendelea kuisaidia jamii yenye mahitaji wakiwemo watoto yatima ili wajihisi kuwa ni sehemu ya jamii inayothaminiwa.

Mkurugenzi mwendeshaji mfuko wa hifadhi ya jamii zanzibar bi Sabra Issa Machano amesema mfuko huo umekuwa karibu na makundi hayo kwa kutambua kuwa wanamahitaji mengi ambayo yanapaswa kuungwa na mkono na taasisi mbalimbali pamoja na wananchi wengine.

Mkurugenzi huyo alikuwa akizungumza wakati wafanyakazi wa ZSSF walipojumuika na watoto yatima wanaoleelwa katika kituo cha mazizini katika futari maalum waliowaandalia pamoja na kutoa msada wa mahitaji mbalimbali.

Kwa upande watoto yatima ambao wameongozwa na msimamizi mkuu wa kituo hicho bi saida ali mohamed amesema kituo hicho kinajisikia faraja kuona kuna taasisi zinawajali watoto yatima, kwani wanahitaji kuwa karibu na jamii muda wote.