ZSTC KUPATA TUNZO NA CHETI CHA UTUNZAJI BORA WA KARAFUU NCHINI UFARANSA

 

 

Shirika la biashara la taifa limefanikiwa kupata tunzo na cheti cha utunzaji bora wa karafuu nchini ufaransa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi uendeshaji wa zstc  said seifamesema zawadi hizo zimetokana na upigwaji wa kura kwa wafanbyabishara elfu saba na mia tano kutoka mataifa tisini wan chi tofauti baada ya kuvutiwa na bidhaa hiyo huku akisema kuwa zawadi walizipata kupitia shirika ni heshima kubwa kwa zanzibar.

Aidha amefahamisha kuwa kutokana na jitihada za serikali ya mapinduzi ya zanzibar ya kulihakikishia zao la karafuu linazidi kuwa bora.

Mkurugenzi wa masoko wa shirika la taifa salum abdallah amewataka wakulima kuwa wasafi zaidi katika kulitunza zao hilo na ili lizidi kupata hadhi siku hadi duniani.