ZSTC WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI KULETA MAENDELEO KATIKA SHIRIKA HILO NA TAIFA

 

Wafanyakazi wa shirika la biashara la taifa zanzibar zstc wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na mashirikiano ili kuleta maendeleo katika shirika hilo na taifa kwa ujumla

Hayo yamesemwa na aliyekuwa mkurugenzi wa utawala wa shirika ndg. Usi mohamed juma katika hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika makao makuu ya shirika hilo maisara mjini unguja.

Amesema wafanyakazi wawanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuondokana na majungu baina yao kwani hakuleti ufanisi wowote na kujitahidi kutatua matatizo na changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi wao.

Naye mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo ndg.khasim maalim suleiman ametoa wito kwa wafanyakazi wote kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ambapo ni miongoni mwa mambo muhimu ili kuleta ufanisi

Pia amesema wanayo mashirikiano mazuri kwa waanguaji karafuu hasa kwa kuzingatia usalama wao katika shughuli zao na shirika limewakatia bima za afya ili kuhakikisha wanapata huduma bora za kiafyan pale wanapopata matatizo ya kiafya