ZURA IMESEMA TATIZO LA UKOSEFU WA MAFUTA ZANZIBAR LILILOTOKEA HIVI KARIBUNI LIMETATULIWA

Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati zanzibar zura imesema tatizo la ukosefu wa mafuta katika mji wa zanzibar lilitokea hivi karibuni limetatuliwa na kuwaomba wananchi kuondoa wasisiwasi juu ya ukosefu wa huduma hiyo.
Mkuregenzi mkuu wa zura haji kali haji amesema kwa sasa nishati hiyo ipo ya kutosha na inaendelea kusambazwa katika vituo vya kuuzia mafuta na kampuni ya gapco.
Akizungumza na waadishi wa habari amesema kuwa kampuni nyengine ikiwemo ya zanzibar petrloeum, puma na united group zina akiba inayoweza kutumika kwa muda mrefu.
Amefahamisha kuwa upungufu uliojitokeza hivi karibuni umetokana na kasoro za kiutendaji na si kama inavyodaiwa kuwa imeruhusiwa kampuni moja pekee kuingiza nishati hiyo.
Katika hatua nyengine mkurugezi kali ameeleza namna ya mamlaka hiyo ilivyobadilisha mfumo mpya wa uingizaji wa mafuta zanzibar alioulezea kuwa unalengo la kupunguza usumbufu wa upatikanaji wa huduma za mafuta kwa wananchi wa zanzibar.