ZURA YATILIANA SAINI YA MKOPO NA MAMLAKA YA MAJI ZAWA ILI KUBORESHA HUDUMA ZA KIJAMII

 

Mamlaka ya udhibiti wa maji na nishati zanzibar zura yatiliana saini ya mkopo  na mamlaka ya maji zawa mkopo wa bilioni moja ili kuboresha huduma mbalinbali za kijamii  ikiwemo umalizaji wa tank la maji  kikwajuni kwa mselemu na ununuzi wa mita za maji ambazo tayari zoezi la ufungaji kwa baadhi ya maeneo umeshaanza .

Wakitiliana saini izo katika ofisi za zura kati ya wakurugenzi wa tasisi hizo mbili mkurugenzi wa zura haji kali haji amesema fedha hizo wanazozikopesha kwa zawa ni kuona tasisi hiyo wanaiwezesha  ili kuona inatoa huduma zilizobora kwa jamii na kuhakikisha zinapatikana bila usumbufu wowote kwani  dira ya mamlaka ya udhibiti wa maji na nishati ni kuwa tasisi ya mfano katika kuunga mkono jitihada za seikali ya mapinduzi ya zbar.

aidha amefahamisha kuwa kwa sasa tank la maji liliopo kikwajuni limesita na harakati za ujenzi na kupelekea baadhi ya wanachi wa kikwaju kukosa huduma ya maji ambayo yanatarajiwa kutokea   katika tangi kubwa la migombani  na kuwafikia waakazi wa eneo la kikwajuni  hivyo basi amewataka wananchi kuwa wastahamilivu zaidi kwani tasisi hizo zimo katika nia thabiti ya kuwaletyea wanachi wake huduma hizo  muhimu .

Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya maji zawa mussa ramadhani haji  amesema kuwa licha ya mamlaka hiyo kuwa na changamoto mbalimbali zawa matarajio yake kuondosha tatizo lamaji nchini huku wakijipanga kuzuia upotevu wa maji kwa asilimia kubwa ya ufungaji wa mita  ili kuondosha malalmiko katika ulipaji  wa maji