Daily Archives: April 16, 2019

UTEKELEZAJI WA KATAZO LA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTI NCHINI NI JAMBO LA MSINGI

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira Mh. Januari Makamba amesema utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plasti Nchini ni jambo la msingi kutokana na faida ziliopo katika utekelezaji wake kwa taifa.

Waziri makamba amebainisha hilo katika kikao cha wadau kuhusu fursa za uwekezaji wa mifuko mbadala kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa julius nyerere jijini dar es salaam.

Amebainisha aina ya mifuko inayopigwa marufuku na kusema kuwa katazo hilo ni mchakato wa muda wa mrefu na si suala la kukurupuka kama baadhi ya wadau wanavyosema.

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Joseph Kakunda ameelezea umuhimu wa mazingira katika sekta ya uchumi na kubainisha madhara ya matumizi ya mifuko ya plastik kiafya.

Angela kairuki ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu anaeshughulikia uwekezaji amewakumbusha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi juu ya fursa zilizopo katika sekta ya utenegenezaji wa vifungashio na kuwahamasisha kuwekeza katika sekta hio.

Kikao hicho cha siku moja chenye lengo la kuhamasisha wadau kuhusu fursa ya uwekezaji na uzalishaji wa mifuko mbadala ili kukidhi mahitaji ya umma pia kimehudhuriwa na naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa raisi balozi sokoine, mkurugenzi wa mazingira Zanzibar, washiriki kutoka sekta binafsi, wajasiriamali, wenye viwanda wafanyabishara ambao kwa pamoja wamekubali kutekeleza agizo hilo la Serikali

VIONGOZI WATAKIWA KUTUMIA HEKMA NA TARATIBU ZA DINI WAKATI WA KUTATUA MIGOGORO

Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar,Khamis Juma Mwalimu, amewataka viongozi wa ofisi ya mufti kutumia hekma na taratibu za dini wakati wa kutatua migogoro ya wananchi.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya mufti ,Wanasheria na Waendesha mashtaka huko katika ukumbi wa ofisi ya DPP Madungu Wilaya ya Chake Chake .

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,George Kazi,amewataka kuacha tabia ya kufunga milango ya ofisi pale jamii inapohitaji kutoa malalamiko yao.

Hata hivyo naye Mwanasheria dhamana ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Pemba, Ali Rajab Ali,amesema ipo haja ya kutoa elimu kwa wananchi  waweze kujua mwenendo wa kesi zinavyokwenda ili kuepuka malalamiko ya Wananchi .

error: Content is protected !!