Monthly Archives: August 2019

SMZ ITAENDELEA KUJENGA MAJENGO YA KIBENKI KILA HALI ITAPORUHUSU

Waziri wa fedha na mipango Balozi Mohammed Ramia amesema serikali  ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kujenga majengo ya kibenki kila hali itaporuhusu ili kuwarahisishia wateja wake kupata huduma kwa urahisi.

Akizungumza wakati akiangalia maendeleo ya ujenzi wa tawi jipya la benki ya watu wa zanzibar huko malindi, amesema ujenzi huo utasaidia kuimarisha upatikanaji huduma bora za kibenki na kuepusha msongomano wa wateja pindi wanapofika kupata huduma.         

Amesema serikali imeridhishwa na hatua za ujenzi huo kwani unaendana na mazingira ya huduma na kuzingatia watu wenye mahitaji maalum

Nae naibu mkurugenzi wa benki ya watu wa Zanzibar PBZ Bi: Khadija Shamte Mzee, amesema benki  hiyo inaendelea kuwasogezea huduma wateja wake ili kuwaondoshea usumbufu wa kufata huduma hizo katika masafa marefu.

 Kwa upande wake msimamizi wa ujenzi huo Bw: Mbaraka Husein inganga amesema jengo hilo ni la kisasa linaloendana na hadhi ya mji mkongwe ambalo litakuwa na huduma zote za kibenki  na  linatarajiwa kumalizika novemba mwaka huu

(ZECO) YARIDHISHWA NA ZOEZI LA UBADILISHAJI MITA ZA ZAMANI

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) limesema hadi kufikia mwezi juni mwakani litakuwa limeshakamilisha zoezi la ubadilishaji mita za zamani na maeneo yote Nchini kuwa na mita za tukuza kutokana na kasi ya ufungaji wa mita hizo kufikia hatua za kuridhisha.

Afisa uhusiano wa ZECO Salum Abdalla Hassan akizungumza wakati wa ufungaji wa mita hizo eneo la kikungwi, amesema kwa wilaya ya kati ni zaidi ya asilimia tisini zoezi hilo limeshafanyika, huku akisisitiza mwamko wa wananchi kutumia huduma za umeme kwani eneo la kikungwi ni miongoni mwa maeneo yaliyofikishwa huduma ya umeme muda mrefu lakini muitikio wa wananchi bado si wa kuridhisha ikizingatiwa kuwa neo hilo lina fursa nyingi za kiuchumi.

Wananchi kwa upande wao wameelezea matumaini yao baada ya kufungiwa mita za tukuza kwani wataondokana na usumbufu pamoja na malalamiko ya mara kwa mara kutokana na mita za zamani

MAAMBUKIZI YA VVU NA UKIMWI KATIKA VYUO VYA MAFUNZO

Msongamano wa watu, lishe duni, upatikanaji mdogo wa huduma za afya na tabia hatarishi zilizomo kwenye vyuo vya mafunzo ni sababu kuu za kuwepo maambukizi ya VVU kama unavyoeleza muongozo wa shirika la afya duniani who juu ya maambukizi ya VVU na ukimwi katika vyuo hivyo.

Muongozo wa shirika hilo, umeifanya Tume ya Ukimwi Pemba kukutana na askari wa vyuo vya Mafunzo Kisiwani humo .

Mratibu wa tume hiyo Pemba Nassor Ali Abdalla akazungumza na kituo hiki na kusema wafanyakazi na wanafunzi wa vyuo vya mafunzo wanakabiliwa na changamoto nyingi.

Aidha mratibu huyo akazungumzia muongozo wa shirika hilo unaotaka sera na miongozo iwalenge wafanyakazi na wanafunzi wa vyuo hivyo.

Mwanasheria wa yuo vya mafunzo Pemba ASP Baraka Mwichum Haji ametoa wito kwa wapiganaji hao kuendelea kutoa taaluma ili kudhibiti maambukizi kwa wanafunzi wa vyuo vya mafunzo.

 

error: Content is protected !!