Daily Archives: September 2, 2019

MABARAZA YA WATOTO YAPATIWA MAFUNZO YANAYOHUSIANA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI

Mkurugenzi  baraza la manispaa Magharibi” B” Nd: Ali Abdalla Natepe amesema baraza hilo limekusudia kuyasaidia mabaraza ya watoto yaliyomo ndani ya wilaya hiyo kwa kuhakikisha linawapatia mafunzo yanayohusiana na vitendo vya udhalilishaji ili kupunguza vitendo hivyo katika jamii.

Natepe ameeleza hayo  wakati akifungua mafunzo ya udhalilishaji dhidi ya wtoto kwa mabaraza ya watoto  ya sehia thalathini na nne za wilaya ya maghribi B yaliyofanyika katika ukumbi wa mnispaa hiyo kwa mchina mwisho.

Amesema endapo mabaraza ya watoto yatasimamiwa  ipasavyo kwa kuwapatia mafunzo ya udhalilishaji yatasaidia kupunguza ongezeko la vitendo hivyo na yataweza kuwajengea mustakabali mzuri wa maisha yao.

Msaadizi mkurugenzi maswala ya mtambuka nd: Abdul Hakim Machano Haji pamoja na afisa ustawi wa jamii  wa wilaya hiyo, Bi: Rukia Abdalla Jaha, wamesema lengo la kuandaa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watoto waliochini ya umri ya miaka kumi  na nane kuhusiana na vitendo vya udhalilishaji na ukatili dhidi yao huku akitoa  wito kwa wazee  kushirikiana kwa pamoja ili kupiga  vita vitendo hivyo.

Wakizungumza kwa  niaba ya watoto wezao mara baada ya kumaliza mafunzo hayo  wamesema kupitia mafunzo hayo yameweza kuwasaidia  kujua haki zao za msingi pamoja na  kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kuhakikisha vitendo hivyo vinaondoka kabisa katika wilaya  hiyo.

 

WAZEE, WALEZI PAMOJA NA WADAU WA MICHEZO WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA

Wazee, walezi pamoja na wadau wa michezo   wametakiwa kushirikiana kuibua vipaji vya vijana vilivyojificha katika michezo hasa maeneo ya vijini kwani  michezo imekuwa ikitoa fursa nzuri ya ajira  na kujikwamua kiuchumi.

Wito huyo umetolewa na mjumbe wa NEC Taifa nd Ramadhani Shaibu Juma  wakati alipokuwa akikabidhi vifa vya michezo na kusherekea ushindi kwa  timu ya fast fast ya  kangangani iliyoibuka na ubingwa katika  kombe la kangangani cup.

Amesema michezo ni ajira endapo vijana hao wataendelezawa vizuri kwa  kutumia vipaji vyao wanaweza kujiri wenyewe kupitia michezo na kuendeleza utamaduni.

Mapema afisa kitengo cha uratibu chama chama pinduzi ccm pemba   mabaye pia ni mlezi wa timu hiyo zulefa abdall said ameipongeza timu ya fasta fast kwa haraka zao za kukimbilia ubingwa kama lilivyo  jina lao    kwa kupata ubingwa huo  kwani mbio za sakafuni hazikuishia ukingoni.

Nao wanachezo wa timu hiyo wamesema licha ya kuibuka na ubingwa huyo ila bado wanakabiliwa na changamoto  mbali mbali ikiwemo ya vifa vya  michezo.

WANANCHI WATAKIWA KUDHIBITI UCHAFUZI WA MAZINGIRA

Viongozi na wadau wa Serikali za mitaa wametakiwa kusimamia majukumu yao ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo yao ili lengo la kuweka mji katika hali ya usafi liweze kufikiwa.

Wito huo umetolewa na katibu tawala Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla Rashid katika mkutano  ulishirikisha viongozi na wadau wa baraza la mji  ya  kuhusu uhifadhi wa uharibifu  mazingira huko ukumbi wa baraza la mji chake chake.

Nae mkuu wa idara ya mazingira Pemba Mwalim Khamis Mwalim ameitaka jamii kuona umuhimu wa uhifadhi wa mazingira  ili kuepukana athari kama vile maradhi ya mitipuko.

Akizungumzia sheria ya serikali za mitaa namba 7 ya 2014  afisa ukaguzi wa afya baraza la mji chake chake khamis machano amesema katika kipengele cha 5 mabano 2 cha sheria hiyo  kinaelekeza kwamba  mtu yoyoyte  atakaezalisha taka  azipeleke katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kukusanyia taka .

error: Content is protected !!