Monthly Archives: February 2020

SERIKALI YA MAPINDINDUZI YA ZANZIBAR IMEPANGA KUKARABATI NYUMBA ZA MICHENZANI

Waziri wa Ardhi Nyumba  Maji na Nishati Mh Salama Aboud Talib amesema Serikali ya Mapindinduzi ya Zanzibar  imepanga kukarabati Nyumba za Michenzani ili Wananchi waishi katika Mazingira bora  yenye usafi ili yaendane na haiba nzuri  ya Mji.

Mh.Salama Aboud ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wanaoishi Nyumba za Michenzani kwenye Uwanja wa Alabama

Amesema kwa sasa wataanza kutengeneza  Nyumba ya Michenza Jumba namba moja ili kuhakikisha Wananchi wanakaa katika mazingira Bora na kuwataka Wananchi hao wanaoishi kutunza Nyumba hizo katika mazingira ya usafi zaidi ili kuwana haiba nzuri ya Mji wenye  kupendeza.

Mkurungenzi  Mkuu wa  Shirika la Nyumba Zanzibar  Nd.Riziki Jecha  Salim amesema   badhi ya Nyumba za Mijiji na Vijiji zimeanza kuchakaa  na kupoteza haiba yake ya asili nakutofata utaratibu kwani wengine hupikia kuni hali inayosababisha uharibifu na kupoteza mandhari ya Nyumba za Michenzani amesema tayari wameanza kukarabati Kisiwa wa Pemba na sasa wataanza Unguja katika Nyumba namba moja.

Baadhi ya Wananchi wameomba  kutengenezewa Makaro ambayo imeonekana ndio yanayosababisha kutokuwa na mandhari mazuri  katika Nyumba za maendeleo ya Zanzibar ili kwenda sambamba na mazingira ya Mji wa Kisasa.

JESHI LA POLISI LIMEAGIZWA KUHARAKISHA KUFANYA UPELELEZI WA KESI

Watendaji wa Jeshi la Polisi wameagizwa kuharakisha kufanya Upelelezi wa Kesi zinazofikishwa katika Vituo vya vyao ili Walalamikaji waweze kupata Haki zao.

Akifunga Mafunzo ya Upelelezi Mdogo kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mkuu wa Ufuatiliaji na tathmini wa Polisi Zanzibar, Naibu Kamishna Mpinga Gyumi amewataka Polisi kutumia Elimu walizonazo ili kufanya Kazi kwa weledi na kuepusha Malalamiko ya Wananchi dhidi ya Jeshi la Polisi kwa kuchelewesha Upelelezi.

Amesema Watendaji wa Jeshi hilo hawana budi kubadilika kwa kutoa huduma bora kwa Wateja wanaofika Vituoni pamoja na kuzingatia vigezo vya makosa ili kuepusha kuwabambikizia Kesi Wananchi.

Nae Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi Emmanuel Jakson Nley amesema mafunzo hayo pamoja na kuwajengea uwezo wa Utendaji pia yamewajenga Kiafya na Kiakili Askari hao.

Mafunzo hayo ya Wiki Sita kuhusiana na Upelelezi mdogo Wamewahusisha Askari 338 kutoka Vituo mbalimbali vya Polisi Tanzania.

 

MABARAZA YA VIJANA 31 YA SHEHIA YA WILAYA YA MAGHARIBI A WAMEKABIDHIWA VIFAA VYA KUFANYIA USAFI

Mabaraza ya Vijana 31  ya Shehia ya Wilaya ya Magharibi A wamekabidhiwa Vifaa mbalimbali  vya  kufanyia Usafi  katika Maeneo mbalimbali ya Mji wa Zanzibar ili kuweka Mji katika Mazingira Safi.

Akikabidhi Vifaa hivyo  vilivyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana  Magharib A Mbunge wa Jimbo la Welezo Mhe Sada Mkuya amesema  Vifaa  hivyo vitawasaidia katika Utendaji Kazi wao   huku akiwataka Vijana hao kuzitumia Fursa zilizopo katika Mabaraza ya Vijana    kwani wao ni nguvu Kazi ya Taifa na pia  wasikubali kutumiliwa    katika  mambo ya  Kisiasa

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Magharib A Rashid Mohd na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar

Khamis Rashid Heri wamesema Vijana wanpaswa  kujielewa  na kujitambua  pamoja na kutuamini michango inayotolewa na Serikali yao .

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Vijana wenzake amewashukuru Viongozi hao kwa kuwakabidhi Vifaa hivyo kwani  vimekuwa vikiwaathiri katika Utendaji Kazi wao kwa vile walivyonavyo ni vichache

Dr.SHEIN AMEZITAKA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA SADC KUWA NA MFUMO BORA WA KUKABILIANA NA MAAFA

Rais  wa  Zanzibar  na  Mwenyekti wa  Baraza  la  Mapinduzi  Dr.Ali  Mohamed Shein  amesema  Nchi  Wanachama  wa  Jumuiya  ya  Maendeleo  Kusini  mwa  Afrika  zianapaswa  kuwa   na  Mfumo  bora  wa  pamoja  wa  kukabiliana  na  Maafa  yanayotokana  na  mabadiliko ya  tabia  Nchi.

Ametoa tamko  hilo wakati  akifungua  Mkutano  wa  wa  kwanza  wa   Kamati  ya  Mawaziri  wenye  dhamana  ya  Menejimenti  ya  Maafa  wa  Nchi  za  SADC  katika  Hoteli  ya  Madinatil Bahari  Mbweni  nje  kidogo  ya  Mji  wa  Zanzibar.

Dr .Shein  amesema  Nchi  za  ukanda  wa   SADC   zimekuwa  zikikabiliana  na  majanga  tofauti  ambayo  kwa  kiasi  kikubwa  yamekuwa  yakichangia  kudhoofisha  uchumi wa  Nchi  hizo  na  umasikini kwa  Wananchi  wake  hivyo  kuwa  na  mkakati  na  mfumo  wa  pamoja  ni  jambo  la  lazima  ili  kuzijengea  uwezo  na  kubadilishana  uzoefu  .

Ameyataaja  majanga  ya  ukame, mafuriko, vimbuinga  na  uvamizi wa  wadudu  katika  mazao ya  kilimo kuwa  ni   changamoto  kwa  Nchi  hizo  inayosababisha  fedha  za maendeleo  kutumika  katika  kurejesha  hali  ya kawaida  baada   ya majanga  na  kusimama  kwa miradi  ya  maendeleo.

Akizungumzia  jinsi  Zanzibar  inavyojiiandaa  juu  ya  kukabiliana  na  Maafa  Rais  wa  Zanzibar  amesema  Serikali  imekuwa  ikiendelea  kuimarisha  mkakati wa  kitaifa  wa  kukabilina  na  Maafa  kwa  kuwajengea  uwezo  Wananchi  ikiwemo  ununuzi wa  Boti  za  kisasa  za  uokozi ,  Drones  pamoja  na  kuwa  na   vituo  Rasmi  vya  uokozi.

Akizungumza  katika  Mkutano  huo  Waziri wa  Nchi  Ofisi  ya  Waziri  Mkuu , Sera ,Bunge  na  Watu  Wenye  Ulemavu  Jennista  Mhagama  amesema  kila  Sekta  hapa  Nchini  inapaswa    kuweka  mkazo  katika  uandaaji  wa  Bajeti  inayoyzingati namna  ya  kukabiliana  na  Maafa,

 

error: Content is protected !!