Recent Posts by asha farouq

WATOTO WAHAMASISHWA KUSHIRIKI CHEMSHA BONGO ZA DINI YA KIISLAM

Wazazi na walezi wametakiwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki kikamilifu katika kujibu masuali mbalimbali ya dini ya kiislamu kwa lengo la kuijua kwa undani dini yao.

Wito huo umetolewa na naibu katibu mkuu anaeshughulikia habari katika wizara ya habari utalii na mambo ya kale Shekhe Saleh Yussuf Mnemo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa chemsha bongo ya ramadhani.

Shekhe Mnemo amesema kipindi cha chemsha bongo ya ramadhani ni chachu ya kuwakumbusha watoto na waislamu kwa ujumla kuifahamu na kuielewa vyema dini ya kiislam.

Nao wafadhili wa kipindi hicho wamewataka watayarishaji wa kipindi hicho kuandaa utaratibu wa kipindi hicho kuonyeshwa ZBC TV.

Akisoma risala ya watayarishaji wa vipindi vya ramadhani Zanzibar Bi Aziza Hassan amesema kipindi hicho kina changamoto nyingi ikiwemo kukosa wafadhili wa kutosha ili   kuwapatia zawadi washindi.

HAKUNA ATHARI ILIYOTOKEA KATIKA SUALA LA UTAFITI WA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Mkurugenzi mamlaka ya mazingira nd.Sheha Mjaja amesema hadi sasa hakuna athari yoyote ya kimazingira iliyotokea katika suala la utafiti wa utafutaji wa mafuta na gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari nd.Mjaja amesema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya idara hiyo na kampuni inayosimamia suala la utafiti wa uchimbaji wa nishati hizo ikiwemo kuzingatiwa zaidi kwa hifadhi za misitu.

Kwa upande wao meneja wa rac gas nd.Damascene makatu na mtendaji mkuu wa rac gas kutoka ras al khaimah,bw.Nishant Dighe,wamesema mchakato wa utafiti wa mafuta na gesizanzibar kwa hatua ya kwanza umekamilika na kinachofanyika ni kutafsiri takwimu kazi ambayo itakamilika septemba mwaka huu.

Waziri wa ardhi,nyumba,maji na nishati Mh.Salama Aboud Talib,amesema suala la utafiti wa upatikanaji wa mafuta na gas ni jambo la muda mrefu hivyo  wananchi ni vyema  kuwa wastahmilivu katika jambo hilo.

JAMII YAPASWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUWASAIDIA WATOTO MAYATIMA

Mkurugenzi wa mfuko wa hifadhi ya  jamii zanzibar zssf nd. Sabra Issa Machano amesema jamii yapaswa kushirikiana  katika kuwasaidia watoto mayatima ili waweze kuishi  kwa furaha na upendo kama watoto wengine

Kauli hiyo ameisema  katika ukumbi wa  viwanja vya kufurahishia watoto kariakoo  wakati akikabidhi  msaada  wa pesa kwa ajili ya watoto mayatima

Aidha  amesema mfuko wa hifadhi ya jamii zssf  inatambua umuhimu wa kuwalea na kuwatunza watoto mayatima . Hivyo  suala la kuwasaidia  watoto mayatima si jambo la hiari bali ni jambo liloamrishwa na mwenyezi mungu  kwa kutegemea malipo siku ya kiama

WAUMINI WAMEOMBWA KUJITOLEA MALI ZAO KATIKA KUZIIMARISHA NYUMBA ZA IBADA

Wakati mwezi mtukufu wa ramadhani ukiwa katika kumi la mwisho, waumini wameombwa kujitolea mali zao katika kuziimarisha nyumba za ibada ambazo ni misikiti kwani fadhila zake ni kubwa kwa mwenyezi mungu.

Hayo yamebainika wakati waumini mbali mbali wakiungana pamoja na wafanyakazi wa shirika la utangazaji zanzibar katika ufunguzi wa msikiti uliojengwa katika kituo hicho kilichopo karume house.

Recent Comments by asha farouq

No comments by asha farouq yet.

Powered by Live Score & Live Score App