Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

MAOFISA WATAKIWA KUTOA MAAMUZI YENYE MASLAHI KWA MAENDELEO YA UWEKEZAJI NCHINI.

Kamati  ya  fedha biashara  na kilimo  ya  baraza la  wawakilishi  imesema  imefarijika  kuanzishwa kwa kitengo  cha  kutoa  huduma kwa  wawekezaji  na wafanyabiashara  ili  kurahisisha  upatikanaji w huduma  kwa  wawekezaji  wa  ndani  na  nje  ya  nchi.

Akiwasilisha  maoni  ya  kamati  yake  kuhusiana na  mswada wa sheria  ya kufuta  sheria  ya  ukuzaji  na  kulinda  vitega uchumi  zanzibar  amesema mswada  huu umeletwa  katika  wakati  muafaka   ili  kuendana na mageuzi  ya  kiuchumi   kutoka  wa  kutegemea  kilmo  hadi  uchumi  wa viwanda   kupitia  wawekezaji tofauti.

Amesema  kamati  imeishauri  wizara au taasisi   zinazopaswa  kushughulikia  kitengo  hicho   kuwa  na  maofisa  wenye  uwezo   wa  kutoa maamuzi  yenye  maslahi kwa  maendeleo  ya  uwekezaji  nchini.

Wakichangia  mswada  huo  wajumbe  wa  baraza  hilo wamesema uwepo wa  mswada  huo utawezesha kuondokana na urasimu  wa  ufuatiliaji  wa  huduma katika  ofisi  mbalimbali  kunakopelekea  kuwavunja moyo  wawekezaji  kuwekeza miradi  yao hapa nchini.

WADAU WANAOPAMBANA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA WATAKIWA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI

Afisa mdhamini ofisi ya makamo wa pili wa rais ali salum mata amewata wadau wanaopambana na matumizi ya madawa ya kulevya kuweka kumbukumbu sahihi ya vitu wanavyivikamata pamoja na kesi zake ili kujua ukubwa wa tatizo hili.

mdhamini mata amesema hayo ofisi za mkurugenzi wa mashtaka chake chake kwenye kikao cha kujadili changamoto za matumizi ya madawa ya kulevya na nini kifanyike, kilichowashirikisha maafisa kutoka zaeca, dpp na polisi.

mkurugenzi wa tume ya kitaifa ya kuratibu na kudhibiti madawa ya kulevya zanzibar kheriyangu mgeni khamis amesema hatua ya kukutana na wadau hao itasaidia kubuni mbinu zitakazoweza kuepusha changamoto dhidi ya tatizo hilo.

wadau wa mapambano hayo walipata nafasi ya kutowa maoni yao.

KESI 32 ZA RUFAA ZINATARAJIWA KUSIKILIZWA KATIKA MAHAKAMA KUU YA VUGA ZANZIBAR

Jumla ya kesi 32 zilizokatiwa rufaa zanzibar  zinatarajiwa  kusikilizwa  katika mahakama kuu ya vuga  iliyopo mjini zanzibar.  Kuanzia  tarehe  26  mwezi huu hadi  tarehe 15 mwezi ujao.

Kesi hizo ambazo zitasikilizwa chini ya  jaji wa mahakama ya rufaa  tanzania Mh  Mbarouk Salum  Mbarouk  zitazihusisha kesi za  rufaa za  makosa ya jinai , kesi za  rufaa za maombi ya madai  na kesi za maombi ya mapitio(civil review)

Jaji wa mahakama ya rufaa nchini tanzania Mh  Mbarouk Salum  Mbarouk  amewaambia waandishi wa habari kuwa   watasikiliza kesi kumi za  aina ya makosa ya jinai,  kesi za rufaa za madai sita ,   kesi kumi na tano za maombi ya madai ( civil  applocation ) na kesi  kesi  moja ya maombi ya mapitio.

Amesema  wananchi hao  wametumia haki zao  za msingi na la busara  kwa kutaka rufaa hivyo amewataka   kujitokeza ili kuitumia haki yao hiyo ya ngazi ya mwisho.

Jaji mkuu wa zanzibar mh omar othman  makungu  amesema   majaji hao wanatajia kusikiliza kesi zote zilizowasilishwa  pamoja   na kutolewa  maamuzi   ya mashauri mazuri katika uendeshaji wake

Powered by Live Score & Live Score App