Category Archives: Michezo na Burudani

YANGA SC IMEZINDUKA BAADA YA USHINDI WA MABAO 2-0 DHIDI YA AFRICAN LYON

Yanga sc imezinduka baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya african lyon jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ushindi huo wa kwanza katika Ligi Kuu ndani ya mechi tatu, wakitoka kufungwa 1-0 na Lipuli na kutoa sare ya 1-1 na Ndanda FC, zote ugenini unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 71 baada ya kucheza mechi 30.

Maana yake, Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya Azam FC waliocheza mechi 30 pia wanaofuatia kwenye nafasi ya pili, mbele ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 57 za mechi 22 tu.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Ebenezer Makambo ambaye yupo katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya kwao.

Bao la kwanza alifunga dakika ya tano ya mchezo akimalizia pasi ndefu ya beki wa kati, Kelvin Patrick Yondan na la pili dakika ya 31 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu wa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’.
Kipindi cha pili Yanga SC iliendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa African Lyon, lakini ikaishia kukosa mabao ya wazi mfululizo.

WASANII NCHINI WAMETAKIWA KUSAJILI VIKUNDI VYAO ILI KUFAIDIKA NA FURSA ZITAKOZOJITOKEZA

Baraza la Sanaa,Sensa ya Filamu na Utamduni Zanzibar limewataka Wasanii mbalimbali Nchini kusajili vikundi vyao ili kufaidika na fursa zitakazojitokeza ndani na nje ya nchi katika kukuza kazi zao.

Akizungumza na wasanii wa Wilaya ya Kati katika mafunzo kwa wasanii hao katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu  na Utamaduni Zanzibar Dk Omar Abdallah Adam amesema ili msanii au kikundi cha wasanii kufikia mafanikio anawajibu wa kujisajili katika taasisi husika kwa ajili ya kunufaika na fursa zinazojitokeza kwa wasanii hao.

Amesema miongoni mwa fursa ambazo msanii anaweza kuzipata baada ya kujisajili  ni kushiriki katika matamasha mbali mbali ya ndani na nje, kukuza kipato cha wasanii na kuweza kupatiwa elimu kwa mujibu wa mabadiliko yaTekenolojia Duniani.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo wameelezea kufurahishwa na mafunzo waliopatiwa kwani yatawajengea uwezo wa kujiamini wakati wa uwasilishaji wa kazi zao  kwa jamii

MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI MPIRA WA PETE IMEZINDULIWA KATIKA KIWANJA CHA GMKANA.

Michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki mpira wa pete imezinduliwa katika kiwanja cha gmkana.

Katika uzinduzi huo umepingwa mchezo kati ya KVZ Zanzibar dhidi ya klabu kutoka Uganda Akiyafunguwa mashindano hayo katibu Mkuu wizara ya vjiana sana,utamaduni na michezo Omar Hassan King amewata wanamichezo kutumia mashindano hayo kujenga umoja na mashirikiano ya kimichezo na sio kujenga uhasama na uadui.

Amesema mashirikiano nchi hizi zinashirikiana katika kila nyanja hasa katika michezo amewataka kukubaliana na matokeo yoyote yanayotokea kiwanjani pamoja na kuyafanya mashindano hayo kuwa na hamasa za kipekee.

Makocha wa timu hizo wamesema ipo haja chama vya mchezo huo kubuni mbinu za kuweza kuunyanyuwa mchezo huo kwa wachezaji.

Katibu wa chama cha mpira wa pete Zanzibar Saidi Ali Mansab amesema kutokuwa na wafadhili wa mchezo huo imebidi chama chao kiitegemee ufadhili wa serikali sehemu kubwa ya mashindano hayo.

error: Content is protected !!