CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA RELI TANZANIA (TRAWU) KIMEKANUSHA TAARIFA ILIYORIPOTIWA

Chama cha wafanyakazi wa reli tanzania (TRAWU) kimekanusha taarifa iliyoripotiwa na moj ya gazatei la nchini kuwa chama hicho kimemdanganya Rais Dkt John Pombe magufuli kwa kumtangaza mtu asiyestahili kuwa mfanyakazi bora.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa reli tanania (TRAWU) taifa lomitu ole saitabau amesema hakuna udanganyifu wowote uliofanyika katika kuwatangaza wafanyakazi bora wa mwaka 2019/2020 siku ya sherehe za mei mosi iliyofanyika katika uwanja wa sokoine mbeya.

Aidha lomitu amesema chama hicho hakihusiki kumchagua mfanyakazi bora bali wao wanaletewa majina kutoka kampuni ya reli tanzania (TCR) na mamlaka ya reli ya tanzania na zambia (TAZARA).

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Nashoni Mariyeri amesema watakutana na chama cha wafanyakazi (tucta) kuangalia jinsi gani wanaweza kufanya ili kuondoa mkanganyiko huo mwakani.

Chama cha wafanyakazi wa reli wa reli tanzania (TRAWU) ni muunganiko wa wafanyakzi wa kampuni ya reli tanzania (TCR) na mamlaka ya reli ya tanzania na zambia (TAZARA).

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App