DK JOHN POMBE MAGUFULI AMEWATAKA WADAU WA SEKTA YA UJENZI KUUNGANISHA NGUVU ZAO

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dk John Pombe Magufuli amewataka wadau wa sekta ya ujenzi kuunganisha nguvu zao  ili kukidhi vigezo vya  kukubalika katika  ushindani wa kupata zabuni.

Rais magufuli ameyasema hayo jijini Dar-es-salaam katika ufunguzi wa mkutano wa majadiliano wa wabunifu wa majengo, waandisi, wakandarasi  na wakadiriaji majenzi  ambapo pia amesema serikali imekuwa ikichukua hatua kuilea  sekta ya ujenzi na miongoni mwa hatua hizo ni kuanzisha bodi   tatu  ambazo ni za usajili wakandarasi, utoaji mafunzo, na usimamizi wa wakandarasi.

Aidha Rais Magufuli  amesema sekta ya ujenzi ni muhimu kwa maendeleo taifa na ni kichocheo cha ukuaji wa sekta nyinginezo za kiuchumi na kijamii na hivyo ni muhimu katika kuiwezesha tanzania kufikia azma yake  ya kuwa Nchi ya viwanda na ya uchumi wa kati.

Naye waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano mhandisi Isack Kamwelwe  akaelezea mafanikio ya sekta ya ujenzi katika ujenzi wa miundo mbinu nchini .

Mwenyekiti wa bodi ya usajili wa makandarasi  mhandisi consolata nginbwa amewaasa wadau wa sekta ya ujenzi kutekeleza majukumu yao kwa weledi  na kukamilisha kazi za miradi kwa ubora zikiwa na thamani halisi ya fedha iliyokadiriwa

Comments are closed.

error: Content is protected !!