DK. MAGUFULI AMEWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI WA WIZARA, MAHAKAMA, MIKOA NA WAKUU WA MAJESHI

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.   Dk. John Pombe  Magufuli  amewaapisha Viongozi  mbalimbali wa Wizara, Mahakama, Mikoa na Wakuu wa Majeshi aliowateuwa hivi karibuni katika nyadhifa mbalimbali.

Hafla hiyo ya Uapisho imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali   akiwemo  Jaji Mkuu wa Tanzania Pro. Ibrahim Juma na Viongozi wa vyama na Serikali, Viongozi wa Dini Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi   na Usalama .

Mapema akiwaapisha Viongozi hao Mh.Rais Magufuli amewataka Wateule hao kufanya kazi kwa Mashirikiano na uadilifu pamoja na kuweka mbele uzalendo kwa maslahi ya Taifa.

Rais Magufuli amesema wote waliowachagulia ni kutokana na sifa za utendaji wao katika nafasi walizotumikia hapo awali ambapo kwa kila mmoja alizitaja sifa na ufanisi wa kazi yake  na hapa anaeleza.

Nae Jaji Mkuu wa Tanzania Pro. Ibrahimu Juma amemshukuru  Rais kwa kuweza kuwajazia safu ya Mahakama kwa kuwapa Viongozi ambao ndio wanahimili kazi za kila siku za Mahakama.

Miongoni mwa Walioapishwa ni pamoja ni Kamishna  Jenerali wa Magereza  Brigedia Generali Suleiman Mungiya Mzee, mwengine ni Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji DCP.Johm William Hausunga.

Wengine   walioapa  ni Msajili Mkuu wa Mahakama Bw. Wilbert  Chuma, Bw. Kelvin Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani na Shamira Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.

Pia amewaapisha Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama akiwemo Jaji Dkt. Gerald, Wakili Julius Kalolo Bundala  na Wakili Genoveva Kato .

Kwa upande wa Makatibu Wakuu waliowapa ni Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Ardhi, Dkt.Hassan Abbas  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Pro.Riziki Silas Shemdoe Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Zena Ahmed Said   Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Nd. Leonard Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.

Pia Rais Dk.Magufuli Amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa ambapo Viongozi hao Walioteuliwa walikula Kiapo cha Uadilifu.

 

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!