HAKUNA ATHARI ILIYOTOKEA KATIKA SUALA LA UTAFITI WA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Mkurugenzi mamlaka ya mazingira nd.Sheha Mjaja amesema hadi sasa hakuna athari yoyote ya kimazingira iliyotokea katika suala la utafiti wa utafutaji wa mafuta na gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari nd.Mjaja amesema mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya idara hiyo na kampuni inayosimamia suala la utafiti wa uchimbaji wa nishati hizo ikiwemo kuzingatiwa zaidi kwa hifadhi za misitu.

Kwa upande wao meneja wa rac gas nd.Damascene makatu na mtendaji mkuu wa rac gas kutoka ras al khaimah,bw.Nishant Dighe,wamesema mchakato wa utafiti wa mafuta na gesizanzibar kwa hatua ya kwanza umekamilika na kinachofanyika ni kutafsiri takwimu kazi ambayo itakamilika septemba mwaka huu.

Waziri wa ardhi,nyumba,maji na nishati Mh.Salama Aboud Talib,amesema suala la utafiti wa upatikanaji wa mafuta na gas ni jambo la muda mrefu hivyo  wananchi ni vyema  kuwa wastahmilivu katika jambo hilo.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App