HALI YA UZALISHAJI WA MBOGA MBOGA BADO IKO CHINI KWA WAKULIMA WA VISIWANI

Hali  ya  uzalishaji wa  mboga mboga  bado  iko  chini    kwa wakulima wa visiwani hivyo wanahitaji kuhamasishwa na kupewa utaalamu zaidi ili kupunguza uagiziaji  wa bidhaa  hiyo  nje  ya  nchi.

Akitoa  maelekezo  kwa  wanavikundi  wa  mboga mboga  mtafiti  kutoka  taasisi  ya  utafiti kizimbani Muhamed  Omar amesema jitihada  za makusudi  zinahitajika  katika  kupambana  na  maradhi  ya  mimea  pamoja  na  matumizi  ya  mbolea  za asili ili kupata  tija  katika  kilimo  chao.

Wakulima  hao  wa  mbogamboga  wameomba kupatiwa  taaluma  zaidi  ya uzalishaji pamoja  na  kukaguliwa mashamba  yao ili  wapatiwe ufumbuzi wa matatizo  walionayo  katika  kilimo.

Mratibu  wa  mradi huo  wa  uimarishaji  wa mboga  mboga  kutoka  chama  cha  malezi  bora  tanzania   umati  Mbarouk  Said amesema  wameamua  kuihamasisha  jamii kuibua  miradi  mbali mbali ikiwemo  ya  ukulima  kwa  kujiongezea  kipato  na  kupunguza  tatizo  la  ajira  kwa  vijana.

Comments are closed.

error: Content is protected !!