IDARA YA MSAADA WA SHERIA IMEBAINI ONGEZEKO KUBWA LA MAHABUSU KATIKA CHUO CHA MAFUNZO KINUA MGUU

Idara ya Msaada wa Sheria Zanzibar imefanya ziara maalum katika Chuo Cha Mafunzo Cha Kiinua Miguu na kubaini ongezeko kubwa la Mahabusu waliokosa dhamana kutokana na sababu mbali mbali.

Chuo hicho kina karibu ya Mahabusu 370  ikilinganishwa na Wafungwa 141 ambapo wingi wa Mahabusu hao wanatuhumiwa kwa  makosa ambayo hayana dhamana Kisheria na kusababisha Gharama kubwa  za  kuwahudumia.

Baadhi  ya  Watendaji wa Taasisi  za  Kisheria wakitoa tathmini ya Ziara hiyo baada  ya  kuwasikiliza Mahabusu na  Wanafunzi  wanaoendelea  na  Adhabu  zao wameshauri kufanyiwa Tathmini ya Kisheria ili kurahisisha utoaji Dhamana .

Mwanasheria Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo SSP Seif Maabadi Makungu ametoa ufafanuzi wa baadhi ya malamiko yaliyotolewa na Mahabusu na Wanafunzi wa Chuo hicho na kueleza kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia haki za Bianaadamu.

Akitoa majumuisho ya Mkurugenzi wa Idara ya Wasaidizi  wa Kisheria Zanzibar Hanifa  Ramadhani amesema ni lazima Watendaji wa Sheria kujitathmini katika usimamizi wa Sheria ili kuwasaidia Watuhumiwa na Wanafunzi waliokuwemo katika Vyuo Vya Mafunzo kwani baadhi wamekuwepo ndani kwa sababu ya kutokufahamu Sheria za kuwalinda.

Ziara  hiyo inaenda sambaba na  Maadhimisho  ya Wiki ya huduma ya  Sheria imewashirikisha Watendaji kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Mahakama Mwanasheria Mkuu Wasaidizi wa huduma zaSsheria na Kituo cha huduma za Sheria Zanzibar.

Comments are closed.

error: Content is protected !!