JAMII IMETAKIWA KUEPUKA KUTUMIA FEDHA TASLIMU WAKATI WA KUFANYA MIAMALA

Jamii imetakiwa kuepuka kutumia fedha taslimu wakati wa kufanya miamala , bali imeshauriwa  kutumia njia za kielektroniki ili kudhibiti uharibifu wa sarafu na noti.

Mkuu wa wilaya ya chake chake Rashid Hadid Rashid ametoa ushauri huo wakati akifungua mkutano wa utambuzi wa fedha halali na haramu , kwa masheha, madiwani wa wilaya hiyo,  pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama.

Amesema ni jukumu la viongozi kusimamia ili kuona sarafu haitumiwi kinyume na utaratibu.

Afisa idara ya sarafu benki kuu , Restituta Magnus ameitaka jamii kuzitunza fedha ili kuisadia serikali kutochapisha pesa mara kwa mara, huku Mkurugenzi mwandamizi wa benki kuu Fidells Mkatte amesema uwepo wa fedha nyingi kuliko mahitaji ya uchumi unasababisha mfumko wa bei.

Kamanda wa polisi mkoa wa kusini pemba kamishna msaidizi mwandamizi Hassan Nassir Ali amesema wanalojukumu la kukataza matumizi haramu ya fedha ambapo Iliyasa Ahmad akishauri benki kuu kuandaa utaratibu kuwadhibiti wananchi wanaotembea na fedha nyingi ndani ya nchi.

Comments are closed.

error: Content is protected !!