JAMII IMETAKIWA KUFAHAMU SHERIA ZA NCHI YAO ILI KUEPUKA KUINGIA MATATANI.

Waziri wa Katiba na  Sheria Zanzibar Mh.Khamis Juma Mwalimu  ameitaka Jamii kufahamu  Sheria za Nchi yao ili kuepuka kuingia katika matatani.

Akizungumza katika  Uzinduzi  wa Maonyesho ya siku ya Sheria  Zanzibar yaliofanyika Viwanja vya  Mnazi  mmoja  Mh.Khamisi amesema Nchi yoyote haiwezi kuendeshwa  bila  ya Sheria kwani bila ya kuwepo Sheria makosa ya uhalifu na uvunjifu wa amani yataongezeka na kuifanya Nchi isikalike.

Amesema Vijana wengi hivi sasa wanajiingiza katika  suala, la  Dawa za kulevya ambalo ndio chimbuko la  kuondezeka kwa vitendo  viovu ukiwemo uhalifu na udhalilishaji .

Jaji Mkuu wa  Zanzibar Mh.Omar  Othmani Makungu  amesema lengo la Maonyesho hayo ni kutoa fursa  kwa  Wananchi kupata  Elimu ya Sheria kwani ni muhimu kwa Jamii kuifahamu.

Siku ya Sheria Zanzibar   hufanyika kila  Mwezi wa Februali ya kila Mwaka ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu  inasema dumisha utawala wa Sheria na Demokrasia  katika Uchaguzi Mkuu 2020.

 

Comments are closed.

error: Content is protected !!